Usiku wa kihistoria kwa Mnyama umewadia, je ataandika rekodi mpya?.
Joyce Shedrack
May 17, 2025
Share :
Klabu ya Simba inatarajia kushuka dimbani usiku wa leo kwenye fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa ugenini dhidi ya RS Berkane katika dimba la Manispaa ya Berkane Nchini Morocco.
Mnyama Simba anaanza safari ya kulisaka taji la kwanza la Afrika ili kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kunyakua taji la Afrika.
Wekundu hao wa msimbazi wanakutana na RS Berkane kwenye dimba lao la nyumbani huku ikiwa ni timu ambayo haijaruhusu goli hata mota msimu huu wakiwa nyumba na wakipata ushindi katika michezo yote.

Matokeo ya Rs Berkane kwenye uwanja wao wa nyumbani msimu huu katika mashindano haya.
Berkane 5-0 Dadje FC
Berkane 2-0 CD Luanda
Berkane 1-0 Stade Malien
Berkane 5- Stellenbosch
Berkane 1-0 Asec Mimosas
Berkane 4-0 CS Constantine.
Je siku ya leo mnyama atavunja rekodi hii na kufanikiwa kutikisa nyavu za RS Berkane ?