pmbet

Utafiti; wanaume wengi wenye matiti makubwa hufa kabla ya kufikisha miaka 75

Sisti Herman

April 15, 2025
Share :

 

Wanaume wenye matiti ambayo yametanuka (gynecomastia), wapo katika hatari ya kufa kabla ya kufika umri wa miaka 75, wanasayansi wamebaini.

Watafiti wamefichua kuwa wanaume ambao wana maradhi kama saratani, matatizo kwenye mapafu ambayo hayajagunduliwa na magonjwa mengine sugu, wapo katika hatari zaidi kufa ikiwa wana matiti ambayo yametanuka.

Mwanaume kuwa na matiti makubwa, husababishwa na kutosawazishwa kwa homoni muhimu ndani ya mwili. Hali hii inawaathiri theluthi mbili ya wanaume wote duniani japo pia hali hiyo inaweza ikawa inatokana na sababu za kiumri.

Watafiti kutoka Denmark kwenye jarida la BMJ Open wamebaini kuwa tatizo la matiti kuwa makubwa kwa wanaume hukolea sana hasa wakiingia uzeeni.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet