Utajiri wa Mo Dewji wapanda, awa wa 12 Afrika
Sisti Herman
March 30, 2025
Share :
Jarida la Forbes (2025) limemtaja Mfanyabiashara wa Tanzania Mohamed Dewji, kuwa miongoni mwa watu matajiri duniani, akiwa na utajiri wa USD 2.2 bilioni sawa na Tsh 5.7 trillioni. Mo, anakuwa tajiri namba 12 Afrika na namba moja Afrika Mashariki kwa utajiri huo.
Orodha ya mwaka huu inaonyesha utajiri wa Mo Dewji umeongezeka na kufikia, dola bilioni 2.2 kutoka dola bilioni 1.8 mwaka jana.
Orodha ya Forbes ya matajiri wa Afrika kwa mwaka 2024 ilibainisha kuwa utajiri wa Mo Dewji umeongezeka kutoka dola bilioni 1.5 hadi bilioni 1.8.
Licha ya utajiri huo, MO Dewji kupitia kampuni ya Mohamed Entrprises Limited (MeTL) imezalisha ajira 40,000 kwa watanzania, kupitia biashara 126 zinazofanywa na kampuni hiyo.
Lengo la Mo Dewji ni kuongeza ajira hadi kufikia laki moja kwa watanzania na wana-Afrika Mashariki.
Mo Dewji kupitia MoDewji Foundation, imeshirikiana na serikali kupitia Wizara ya Maji, kuchimba visima, kukarabati na kutibu maji mkakati uliosaidia watu zaidi ya 15,000 kupata maji salama ya kunywa.
Utajiri wa Mo Dewji haikushia kwenye maji na afya pekee, umekwenda zaidi na kuwekeza katika tasnia ya michezo ambako ni sehemu ya mmiliki akiwekeza asilimia 49 kwenye klabu ya Simba.