pmbet

Vibe la Mpanzu mazoezini Simba ni hatari

Sisti Herman

October 4, 2024
Share :

Ikiwa ni siku mbili tu tangu atambulishwe kuwa mchezaji mpya wa klabu ya Simba, kiungo mshambuliaji raia wa Congo DR Ellie ameanza kwa ari kubwa mazoezi baada ya kujumuika na wenzake kambini huku picha mbalimbali zilizochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo zikimuonyesha akishangilia magoli mazoezini.

Mashabiki wengi wamekuwa na shauku kubwa ya muona mchezaji huyo ambaye hata hivyo hatoweza kucheza ligi kuu Tanzania bara kwasasa hadi atakaposajiliwa kwenye mifumo ya usajili ya dirisha dogo.

Mpanzu anaweza kujumuishwa kuwa mchezaji wa Simba kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ambayo droo ya hatua ya makundi inatarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Simba leo watashuka dimba la KMC Complex kuvaana na Coastal Union kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa kuanzia saa 10 jioni. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet