pmbet

Vibenten vinanisumbua sana, yaani sijui kwa nini? – Binti Msumi

Eric Buyanza

June 12, 2025
Share :

Amina Kombo au maarufu kwa jina la ‘Binti Msumi’ ni mmoja wa nyota wa Bongo Movie walioteka hadhira kubwa. Amejipatia jina hasa kutokana na kuigiza kama mke wa Mzee Kikala katika Tamthilia ya Kombolela.

 

Kwenye mahojiano na Mwanaspoti hivi karibuni, Amina anaulizwa swali kuhusu kupenda Vibenten na hivi ndivyo alivyojibu.

 

SWALI: Uliwahi kuigiza unapenda vibenten, vipi kwenye maisha ya kawaida?
 

BINTI MSUMI: Kwenye maisha ya kawaida mimi sipo hivyo ila kwa jinsi nilivyoigiza nilipata usumbufu wa wavulana wadogo wengi wakidhani ndiyo nilivyo.

 

Tamthilia ilikuwa inaitwa Vibenten, basi hivyo Vibenten vinanisumbua sana, yaani sijui kwa nini. Unakuta kijana kidogo kinakuja huku linang’ata ng’ata mdomo, mie naomba wanikome tu.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet