pmbet

Victor Osimhen ashindwa kupangua Mabilioni ya AL Hilal.

Joyce Shedrack

June 7, 2025
Share :

Klabu ya AL Hilal ya Saudi Arabia inaripotiwa kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kupata huduma ya mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Nigeria na klabu ya Napoli anayeitumikia Galatasaray ya ligi kuu Uturuki kwa mkopo Victor Osimhen.

Victor Osimhen agrees to join club - centredevils

Baadhi ya taarifa zinaripoti kuwa mshambuliaji huyo tayari ameikubali ofa aliyopewa na klabu hiyo ya Saudi Arabia ambao msimu ujao kikosi chao kitakuwa chini ya kocha Simone Inzaghi.

 

Nyota huyo msimu uliopita amefunga magoli 26 na kutoa pasi 5 za magoli katika michezo 30 ya ligi kuu Uturuki huku akifanikiwa kuwa mshambuliaji bora wa ligi hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet