pmbet

Vita ya ubingwa ligi kuu ya wanawake yazidi kunoga JKT Vinara.

Joyce Shedrack

May 14, 2025
Share :

Klabu ya JKT Queens imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya wanawake kufuatia ushindi wa magoli 2-0 walioupata siku ya leo dhidi ya Yanga Princess.

JKT Queens wamekusanya alama tatu zilizofufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa ligi huku wakimshusha mpinzani wao mkubwa Simba Queens na kukaa kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya magoli 16 wote wakiwa na alama 41.

 

Timu zote mbili zimebakiza michezo miwili ili kutamatika kwa msimu huu Simba Queens imebakiza michezo miwili dhidi ya Bunda Queens na 
Alliance Girls wakati JKT Queens ikibakiwa na michezo miwili pia dhidi ya Fountain Gate Princess na Gets Program.

 

Nani kuibuka bingwa wa ligi kuu ya wanawake msimu huu ?

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet