Waarabu wanainyatia saini ya Bruno Fernandes baada ya kumkosa Salah.
Joyce Shedrack
May 6, 2025
Share :
Kiungo wa Machenster United na Timu ya Taifa ya Ureno Bruno Fernandes anatajwa kuwa kwenye mawindo ya klabu ya AL Hilal ya Saudia Arabia katika dirisha kubwa la usajili.

Taarifa kutoka Saudia Arabia zinaripoti kuwa klabu hiyo imetenga fedha nyingi kwa ajili ya kunasa saini ya nyota huyo baada ya kumkosa mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah ambaye amechagua kusalia Anfield.
Hata hivyo Manchester United haina mpango wa kumuuza nyota huyo kutokana na kuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi kinachonolewa na kocha Ruben Amorim aliyefunga magoli 19 na kutoa pasi 18 za magoli msimu huu.
Mpaka sasa hakuna ofa maalum iliyopelekwa mezani mwa Man U kutoka kwa Al Hilal ila ripoti zinasema kuwa wawakilishi wa Bruno walifanya mazungumzo na Al Hilal siku ya jumatatu.
Bruno ambaye alijiunga na Mancher United mwaka 2020 bado ana mkataba wa kusalia klabuni hapo hadi mwaka 2027.