pmbet

Waasi wa M23 wakana kuua raia katika jimbo la Kivu

Eric Buyanza

August 11, 2025
Share :

Waasi wa M23 wanaodhibiti maaneo ya mashariki mwa DRC wamekana madai ya kuua raia katika jimbo la Kivu Kusini pamoja na madai ya kuajiri askari watoto.

Msemaji wa M23 , Willy Ngoma ameiambia BBC kuwa sio lengo lao kuwalenga raia.
"Hatuui raia ... Tunawezaje kuua raia ambao tunapaswa kuwalinda? Hatuwezi hata kuua kuku wao... tunaheshimu raia," anasema Ngoma.

Jeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hivi karibuni lilishutumu kundi la M23 kwa mauaji hayo baada ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kusema imepokea ushahidi wa moja kwa moja za kwamba zaidi ya raia 300 waliuawa mwezi uliopita na waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda.

Ngoma anasema kuwa Umoja wa Mataifa huko kuona hali halisi katika maeneo ambayo M23 inadhibiti na kwamba wamekuwa wakipokea maoni na taarifa zenye msimamo mkali kutoka kwa serikali ya DRC.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet