Wachezaji Simba hawakati tamaa wana tabia za kishujaa - Fadlu
Eric Buyanza
December 26, 2024
Share :
Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amewasifia wachezaji wake akisema wana tabia za kishujaa kwa sababu hawakati tamaa na wamejijengea tabia ya kucheza kwa kupambana mpaka filimbi ya mwisho.
"Wachezaji wangu wameonesha fikra za kutokata tamaa, wanacheza kama mashujaa, wanapambana na kutokata tamaa hata kama dakika zinaelekea kumalizika, hata mashabiki wetu sasa wanapaswa kuwa na utamaduni kama wa wachezaji wao, kutokata tamaa hadi mwisho, hiki ndicho ninachotengeneza kwenye timu" amesema Fadlu.
👉NIPASHE