Wafanyakazi wa ndani wa kenya 'Wanabakwa' nchini Saudi Arabia
Eric Buyanza
May 13, 2025
Share :
Shirika la Amnesty International limesema wafanyikazi wa nyumbani raia wa Kenya walioko Saudi Arabia wanapitia hali za mateso ikiwa ni pamoja na kufungwa, ubaguzi wa rangi na mara nyingine kubakwa.
Katika ripoti yao iliyotolewa leo Jumanne, Amnesty International imeongeza kuwa masharti ya kazi kwa Wakenya hao ni ya kikatili kiasi cha kufikia kiwango cha kile walichokiita "kazi ya kulazimishwa na usafirishaji haramu.”
Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limeeleza kwa kina hali ya mateso wanayopitia zaidi ya wanawake 70 waliokuwa wakifanya kazi za nyumbani nchini Saudi Arabia.
Wafanyikazi wao wa ndani wanatajwa kupitia hali mbaya za maisha na unyanyasaji wa kibinadamu ikiwa ni Pamoja na ukatili wa kingono, matusi na vipigo.
Amnesty International pia imesema serikali ya Kenya inahusika moja kwa moja katika unyonyaji huo wa wafanyakazi.
Ripoti hiyo imetolewa wakati Rais wa Marekani Donald Trump akitarajiwa kufanya ziara rasmi leo mjini Riyadh.
DW