Wakili Peter Madeleka rasmi ni mwanachama wa ACT Wazalendo.
Joyce Shedrack
May 20, 2025
Share :
Wakili mashuhuri nchini Tanzania, Peter Madeleka ametambulishwa kuwa Mwanachama mpya wa Chama Cha ACT Wazalendo, leo Mei 20, 2025 wakati wa hafla fupi ya kumtambulisha iliyofanyika Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.
Wakili Madeleka amekabidhiwa kadi ya Chama hicho na Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita ambapo pia ameingia katika Idara ya Sheria ya chama hicho.
Madeleka alikuwa akihusishwa kuwa ni kada wa CHADEMA, ambapo leo ameeleza kuwa hapo mwanzo alikuwa ni Mwanaharakati huru na sasa ndiyo ameingia kwenye siasa kama Mwanachama wa chama cha siasa.