Walimdanganya mwalimu au wamepona? - Mzee wa Jambia
Eric Buyanza
June 5, 2025
Share :
Maswali ni Mengi as to why wachezaji ambao Mwalimu Hemmed Suleiman Morocco alitangaza kutowaita Kwasababu ni Majeruhi siku Chache Baadae wanaonekana Kwenye Mazoezi ya Klabu zao?..
Walimdanganya Mwalimu wa timu ya Taifa ili wabaki Kwenye Klabu zao au Wamepona hizo siku Chache baada tu ya Taifa Stars Kuwa tayari Imesafiri?
Mudathir Yahaya,Clement Mzize ndo walitangazwa Kutoitwa Sababu ya Majeraha na wanaonekana wanafanya Mazoezi Kawaida na Ofisa habari wao Ali Kamwe akimtamgaza Yao Yao Kuwa Majeruhi Pekee
Shomari Kapombe aliitwa na Akaripoti Kambini Lakini aliomba Kuachwa Kwasababu bado hajapona tangu alipokosa Mechi dhidi ya Singida black Stars.
Ninachotaka Kuamini ni Kwamba hawa wachezaji Kweli walikuwa na Majeraha na katika namna ya Kushangaza wamepata ahueni Mara tu baada ya Stars Kuwa imesafiri.
Ameandika @mzeewajambia mchambuzi wa @efmtanzania