pmbet

Waliotekwa wamerudishwa kwa familia zao - Ruto

Eric Buyanza

May 13, 2025
Share :

Rais wa Kenya William Ruto amesema watu wote waliotekwa nyara kufuatia maandamano ya kupinga serikali mwaka jana wamerejeshwa kwenye familia zao, na akaahidi tukio hilo halitajirudia tena. 

Akizungumza na waandishi wa habari hapo jana mbele ya mgeni wake Rais wa Finland, Alexander Stubb, Ruto alisema: 

"Wote waliotekwa au kupotea wamepelekwa nyumbani kwao na nimeelekeza kwa uwazi kabisa kwamba jambo kama hilo halitarudiwa tena nchini Kenya.”

Ruto alisema tangu alipoingia madarakani mwaka 2022, aliahidi kuondoa tabia ya siasa za utekaji na mauaji ya kiholela ambayo yamekithiri nchini humo kwa miaka mingi. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet