Walker astaafu kucheza timu ya taifa Uingereza
Sisti Herman
March 11, 2026
Share :

Kyle Walker ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa akiwa na timu ya taifa ya Uingereza kabla ya Kombe la Dunia la FIFA.
Kyle (34) anaondoka Three Lions baada ya kucheza mechi 96, akiiwakilisha Uingereza katika michuano mitano mikubwa na kulisaidia taifa hilo kufika fainali mbili za kimataifa.





