Wamuache mwanangu atulie kwenye ndoa yake – Khadija Kopa
Eric Buyanza
June 17, 2025
Share :
Nyota wa Bongo Fleva, Zuchu amesema watu wajiandae kwa pati la baada ya ndoa na siku hiyo watu watakula na kunywa, huku mama yake, Khadija Kopa akiwa akiwafunga midomo waliokuwa wakiwagombanisha na wakwe zao.
“Unajua mimi na mume wangu Diamond tulikuwa hatujaamua kuweka wazi tu ndoa yetu au kufanya sherehe kwa sababu tumekaa pamoja muda mrefu sana, yaani kisheria ni mke na mume, ila kuhusu sherehe baada ya kufunga ndoa, siwezi kusema ni lini, lakini watu wasubiri sherehe ipo na watapewa taarifa,” alisema Zuchu, huku Khadija Kopa akiongeza kwa kuwataka watu waache kumzulia mwanae kwa kudai haelewani na Mama Diamond ikiwa hawana uhakika.
"Sasa wamuache mwanangu atulie katika ndoa yake, maana wamemsema sana, mara king'ang'a, mara hapendwi na mkwe wake, sasa hapendwi wao waliona wapi huyo mkwe wake ametamka hayo maneno? Wasitake kuwagombanisha maana wameshindwa katika ndoa wamezua ya kutopendwa ukweni," alisema Khadija Kopa ambaye ni nyota wa muziki wa taarabu nchini.
MWANASPOTI