pmbet

Wanadiplomasia wawili wa EU watimuliwa Burkina Faso

Eric Buyanza

July 16, 2026
Share :

Mamlaka Nchini Burkina Faso imetoa saa 72 kwa wanadiplomasia wawili wa Umoja wa Ulaya kuondoka nchini humo. 
Wanadiplomasia hao wametajwa kama watu wasiotakikana na kutakiwa kuondoka mara moja.

 

Wanadiplomasia hao ni mjumbe wa EU, aliyetajwa kama Mkuu wa Kitengo cha Siasa, Habari na Vyombo vya Habari nchini humo.

 

Mwingine ni Ofisa anayesimamia miradi na programu mbalimbali za maendeleo za Umoja wa Ulaya nchini Burkina Faso.

 

Utawala wa kijeshi haujatoa maelezo yoyote kufafanua hatua hiyo, ila imekuja  baada ya hapo mwezi Juni Bunge la EU kupitisha  hoja iliyokosoa utawala wa kijeshi nchini Burkina Faso kuminya uhuru wa raia kujieleza, kufanya ukamataji wa kiholela na kukithiri ukiukaji wa haki za binadamu nchini humo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet