pmbet

"Wanatuonea wivu sisi kuwa hapa" Ahmed Ally.

Joyce Shedrack

April 4, 2025
Share :

“Tuna kila sababu ya kujivunia kuwa Simba, tuna kila sababu ya kujivunia kuwa peke yetu katika Kombe la Shirikisho Afrika, tuna kila sababu ya kujivunia kuwa wawakilishi wa nchi kimataifa"Amesema Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba.

Ahmed Ally: Bado Nafasi ya Ubingwa Tunayo – Global Publishers
"Ndio mnaona tunahamasishana kuja Uwanja wa Mkapa, watu ambao hawana shughuli ndio mnaona wanatukana viongozi wa serikali. Sisi tuko busy kuhakikisha mpira wa Tanzania unasonga mbele.”

“Wanatuonea wivu sisi kuwa hapa. Sasa niwambie yeyote ambaye atatia mkono kwenye hili aache ameandika wosia kwenye familia yake.

"Kama wanadhani tunatania basi tutakutana safari hii. Hii mechi tunaitaka, na tunaitaka sana. Tayari tumeshacheza robo fainali tano, hii ya sita tunataka kwenda nusu fainali. Al Masry watake wasitake tutaenda. Safari hii hatuishii robo fainali. Tunasema kwa kauli moja HII TUNAVUKA.” @ahmedally_ .


 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet