Wanaume wajitokeza kupima saratani ya matiti
Eric Buyanza
October 18, 2025
Share :
Wanaume wamejitokeza kwa wingi kupima saratani ya matiti baada ya kupata mafunzo ya kina kuhusu ugonjwa huo, ikiwemo chanzo chake, dalili, na njia za kinga na matibabu.
Mafunzo hayo yametolewa jana Oktoba 17 jijini Dar es Salaam, na Asasi isiyo ya kiserikali ya (JHPIEGO), kupitia mradi wake wa kupambana na saratani ya matiti, unaolenga kuongeza uelewa na kuhamasisha uchunguzi mapema miongoni mwa jamii.
Washiriki wameeleza kwamba mafunzo hayo yametoa mwanga mpya kuhusu umuhimu wa kujitunza na kuhamasisha familia na marafiki kuhusu uchunguzi wa awali, hatua muhimu katika kupunguza vifo vinavyosababishwa na saratani ya matiti.
TSN