pmbet

Watu 20 wafariki kwa ajali ya jengo lililoporomoka Kariakoo.

Joyce Shedrack

November 20, 2024
Share :

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hadi kufikia leo saa 3 asubuhi idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ajali ya kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo jijini Dar es Salaam imefikia 20.

Rais Dkt. Samia amesema hayo leo Novemba 20, 2024 Baada ya kutembelea eneo la ajali Kariakoo.

"Lengo letu kubwa lilikuwa ni kuokoa wenzetu walionaswa ndani ya jengo lile wakiwa hai, lakini kama tunavyoambiwa jitihada haiondoshi kudra ya Mungu, pamoja na jitihada iliyofanywa na serikali na waokoaji lakini bado kuna wenzetu ambao tumewapoteza.

"Na kwamba mpaka saa 3:00 asubuhi leo tumepoteza wenzetu 20,"Rais Samia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet