pmbet

"Watu watatembea bila nguo kwa kuchanganyikiwa" - Ahmed Ally

Eric Buyanza

May 30, 2025
Share :

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amendika hiviii;

Kurwa aliandika barua ya kujilizaliza

Jana Kamshawishi Doi nae aandike malalamiko tena aweke na vitisho eti atajitoa kwenye mashindano, Yaani Doi nae anatishia watu, timu ina miezi sita tangu ianzishwe na yenyewe inaitishia mamlaka

Wameona haitoshi sasa wanawatumia Vibaraka wao kwenye Media kuhamasisha mgomo kwa Vilabu vingine

Vibaraka bila hata kupima ukweli wa jambo wanatoa taarifa Vilabu sita vimeandika Malalamiko na hawatocheza mechi zilizobaki bila hata kutaja vilabu husika

Yaani afungwe Doi halafu Azam aandike Malalamiko au afungwe mbadilisha majina kila siku halafu JKT asusie ligi??

Sisi tutaendelea kushinda mechi kadri Allah anavyotujaalia na kadri tunavyokua bora kiwanjani siku husika

Bodi ya Ligi na TFF endeleeni kusimamia haki, msisikilize kelele za Wapagazi wasiokubali kushindwa na kukubali kuwa msimu huu Simba ni bora

Waamuzi msiyumbishwe na kelele za wanaotaka kuwatia presha mharibu kazi yenu, pigeni kazi simamieni sheria za mpira

Hii ni Ubaya Ubwela Phase One, Tutakapoingia Phase Two watu watatembea bila nguo kwa kuchanganyikiwa

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet