Waziri mkuu wa Kongo aenda jela miaka 10
Eric Buyanza
May 21, 2025
Share :
Waziri mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Augustin Matata Ponyo amehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela na kazi ngumu baada ya kutiwa hatiani kwa ufisadi.
Kufuatia mapambano ya kisheria yaliyodumua kwa takriban miaka minne, mahakama ya katiba ya Kongo imemkuta Matata na hatia kwa ubadhirifu wa fedha za umma za thamani ya Dola milioni 247.