pmbet

Wizara ya Afya yabaini ongezeko la wagonjwa wenye Covid-19,Dar.

Joyce Shedrack

May 20, 2025
Share :

Wizara ya Afya nchini imetoa wito kwa wananchi kuzingatia kanuni za afya ili kujikinga na kuwalinda wengine dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa.

Coronaviruses (COVID-19) – NFID
Wito huo umetolewa leo na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, baada ya ongezeko la tetesi zinazohusiana na magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa katika jamii hususani mkoa wa Dar es Salaam kati ya Mwezi Januari hadi Aprili 2025.

Kupitia taarifa hiyo, Dkt. Magembe amesema kuwa vipimo vya maabara vimebaini kuongezeka na kupungua ambapo amesema kumekuwepo ongezeko la tetesi zinazohusiana na magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa katika jamii nchini.

Dk Magembe amesema kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya mfumo njia ya hewa, wizara imebaini kuna ongezeko la wagonjwa wenye Uviko-19 kutoka wawili kati ya watu 139 waliopimwa Februari sawa na asilimia 1.4 hadi wagonjwa 31 kati ya watu 185 waliopimwa Aprili mwaka huu, sawa na asilimia 16.8.

“Tangu Februari hadi Aprili 2025, ufuatiliaji wa virusi hivi umeonesha ongezeko la visa vya UVIKO-19 kutoka asilimia 1.4 (wagonjwa wawili kati ya watu 139 waliopimwa) Februari hadi asilimia 16.3 (wagonjwa 31 kati ya 190 waliopimwa) Machi,” amesema Dk Magembe.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet