Yanga yampa pole Boka kwa kufiwa na Baba yake mzazi
Sisti Herman
January 13, 2025
Share :
Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, Klabu ya Yanga imetoa pole kwa mchezaji wake, Chadrack Boka kufuatia kufiwa na baba yake mzazi.
Ujumbe wa kumpa pole Boka unasomeka:
"Uongozi wa Young Africans Sports Club tunapenda kutoa pole kwa mchezaji wetu Chadrack Boka, kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi kilichotokea Tarehe 11/01/2025, nyumbani kwao Kinshasa DR Congo.
"Uongozi wa Young Africans unaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na unawataka wanafamilia wote kuwa na subira.
"Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina."