Yanga yamtangaza kocha wa Sindida kuwa mrithi wa Ramovic
Sisti Herman
February 5, 2025
Share :

Klabu ya Yanga imetambulisha aliyekuwa Kocha mpya wa klabu ya Singida Black Stars Hamdi Miloud mwenye Uraia wa nchi mbili za Ufaransa na Algeria kuwa kocha mkuu wa klabu yao kurithi mikoba ya kocha Sead Ramovic.
Kocha Hamdi aliyejiunga na Singida wiki chache zilizopita ana rekodi nzuri ya kufika Hatua ya Fainali katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League - Finals), Robo Fainali mara mbili Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL Quarter Finals) na Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC Quarter Finals).
Vilevile, Kocha Hamdi ana uzoefu mkubwa na Soka la Afrika kwa kuzinoa klabu mbalimbali kwa mafanikio makubwa barani Afrika zikiwemo USM Alger na JS Kabylie za Algeria, Al- Salmiya ya Kuwait, TP Mazembe ya Congo, Athletico Marseille na ES Vitrolles za Ufaransa na Al- Ettifaq FC ya Saudia Arabia.





