Yanga yarahisishiwa na CAF kuwaua wa MC Alger Algeria.
Joyce Shedrack
November 25, 2024
Share :
Klabu ya Yanga imepata unafuu kwenye mchezo wao wa Klabu bingwa barani Afrika dhidi ya MC Alger utakaopigwa Desemba 7 Nchini Algeria kufuatia adhabu waliyoipata Mc Alger kutoka Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kupitia Kamati ya Nidhamu ya kucheza bila uwepo wa mashabiki uwanjani kwenye mechi zao nne za nyumbani za michuano ya CAF.
MC Alger ambao wapo kundi moja na klabu ya Yanga ,Al Hilal ya Sudan na TP Mazembe imekumbana na adhabu hiyo kutokana na vitendo visivyoridhisha vya mashabiki wa timu hiyo wakati wa mechi ya kufuzu hatua ya makundi dhidi ya US Monastir uliopigwa septemba 21,2024 Nchini Algeria.
MC Alger imekumbana na adhabu ya kucheza mechi zao nne za nyumbani za michuano ya CAF bila mashabiki, huku kukiwa na masharti ya kutofanya kosa lolote ndani ya miezi 12 ijayo.