Young Killer amjibu Chid Benz.
Joyce Shedrack
January 23, 2026
Share :
Rapa Young Killer amemjibu msanii mwenzake Chid Benz kufuatia kauli aliyotoa siku chache zilizopita akidai kuwa kuna jambo ambalo Young Killer alimfanyia hakupendezwa nalo.
Hata hivyo, wakati Chid Benz akieleza kutoridhishwa kwake, hakuelezwa wazi ni jambo gani hasa lililotokea kati yao, hali iliyoacha mashabiki na wadau wa muziki wakiwa na maswali mengi.
Leo, kupitia ukurasa wake wa Instagram Young Killer ameweka wazi msimamo wake kwa kuandika ujumbe uliosisitiza heshima na mapenzi, akisema:
“Kilichomo ndani yangu kuhusu wewe Big brother ni respect na big love, ila kama unatafsiri tofauti na hivyo, unanikosea kaka Chid Benz"
Kauli hiyo ya Young Killer imeonekana kama jaribio la kupunguza mvutano na kuweka wazi kuwa hana nia mbaya dhidi ya Chidi Benz, akimtaja kama “big brother” na kusisitiza heshima aliyonayo kwake.





