pmbet

Zanzibar kuanzisha shirika la ndege

Sisti Herman

June 10, 2025
Share :

 

Zanzibar iko kwenye majadiliano ya kina na wawekezaji watarajiwa huku ikiendelea na mipango ya kuanzisha shirika la ndege la taifa. Mpango huu unatazamwa kama hatua ya kimkakati ya kuimarisha uhusiano wa visiwa na uwezo wa utalii.

Katika kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar kilichofanyika Chukwani, naibu waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Nadir Abdulatif Yussuf alitangaza maendeleo hayo Jumatatu.

Alifichua kuwa serikali kwa sasa iko kwenye majadiliano na EgyptAir, ikiwa tayari imefikia makubaliano ya awali ya kuchunguza uwezekano wa kuzindua shirika hilo.

"Mazungumzo na EgyptAir yanaendelea, na tumeanzisha makubaliano ya awali ya mfumo wa kuunda shirika la ndege la Zanzibar," alisema Bw Yussuf akijibu maswali ya wajumbe wa Baraza.

Kauli yake hiyo imekuja baada ya mbunge wa Mtambwe, Dk Mohamed Ali Suleiman kuitaka serikali kuangalia iwapo ni wakati muafaka wa kutekeleza mkakati wa muda mrefu wa kuanzisha shirika la ndege la Taifa Zanzibar.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet