pmbet

Zumaridi matatani kwa kuendesha shughuli bila kibali

Eric Buyanza

May 16, 2025
Share :

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limemkamata Diana Bundala (42) maarufu Zumaridi, kwa tuhuma za kuendesha shughuli za kidini bila usajili rasmi na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa Mtaa wa Buguku, Kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa, imesema kuwa Zumaridi amekamatwq Mei 15, 2025 majira ya saa nne asubuhi .

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Mtafungwa mbali na Zumaridi kutuhumiwa kuendesha shughuli za kidini bila kusajiliwa pia anahusishwa na video inayosambaa mitandaoni ikimuonyesha akiwa na kundi la watoto wa kike na wa kiume huku akidai kuwa yeye ni Mungu wao na ana uwezo wa kuwalinda dhidi ya kifo.

“ Uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na taasisi nyingine za serikali, tunawaomba wananchi wenye taarifa mbalimbali kusaidia uchunguzi watoe ushirikiano ili hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa mara tu uchunguzi utakapokamilika, imeleeza taarifa ya Kamanda.

Sio mara ya kwanza Zumaridi kukamatwa na Jeshi la Polisi, mwaka 2022 alituhumiwa kwa usafirishaji haramu wa binadamu 149.

NIPASHE

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet